KESI YA BINTI ALIYEBAKWA NA KULAWITIWA NA VIJANA WA AFANDE YAANZA KURINDIMA

0

Watu wanne ambao wanatuhumiwa kutumwa na afande kumdhalilisha binti wa Yombo Dovya Jijini Dar es salaam wamefikishwa mahakamani Leo Agosti 19, 2024 na kusomewa mashktaka mawili ya kubaka kwa kikundi (gang rape) na kumwingilia kinyume na maumbile binti ambaye hakutajwa jina lake mahakamani.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama kuu ya Tanzania Mkoani Dodoma Mkurugenzi msaidizi kutoka Ofisi ya Mashtaka Makao Makuu, Renatus Mkude amesema vijana hao wamekana mashtaka hayo na kutokana na unyeti wa shauri hilo wataendelea kuwa mahabusu huku shauri lao likisikilizwa kwa siku tano mfululizo.

Watuhumiwa hao waliofikishwa mahakamani ni MT. 140105 Clinton Honest Damas maarufu Nyundo,Amin Lord Lema ,Nickson Idala Jackson na C.1693 Playgod Edwin Mushi huku jina la binti aliyefanyiwa ukatili huo kutotajwa mahakamani ili kulinda utu wake kwa mujibu wa sheria za nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *