ACTION AUTO GARAGE YAFUNGULIWA DODOMA

0

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule Leo Agosti 15/2024, amezindua karakana ya kisasa ya Toyota ( Action auto Garage) inayojihusisha na utengenezaji wa kisasa wa magari inayopatikana Nzuguni Jijini Dodoma.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Senyamule amewataka madereva wa magari kupatiwa Elimu Ili kuepusha uharibifu na kuzuia uchakavu wa vyombo hivyo unaotokana na Uzembe.

“Mkurugenzi wa Garage hii amesema madereva wanatakiwa waje wapate Elimu, kwa hiyo nisisitize jambo hili Kwa Taasisi zote za Serikali na watu Binafsi, Magari haya yana gharama kubwa sana kwa hiyo tunategemea yakae muda mrefu lakini ukiona yamekaa muda mchache ujue kuna tatizo mahali na matatizo mengi unakuta si ya mtengenezaji ila ni ya kwetu kwa sababu ya kutofuata maelekezo ya matumizi husika ikiwemo kufanya Service Kwa wakati kwa hiyo inatakiwa upatiwe Elimu ya kutosha”, Mhe. Senyamule

Aidha Mhe. Senyamule amewapongeza Toyota Tanzania Kwa kufungua Chumba Cha maonesho ya magari Mkoani Dodoma kwani Kwa kufanya hivo kunawarahisishia upatikanaji wa huduma hiyo Kwa wakazi wa Mkoa huo na Mikoa Jirani

“Mimi furaha yangu ni kuwa tulizoea kuyapata magari haya mapya kutoka Mikoa mingine lakini sasa tunaanza kupata hapa hapa, unachukua ufunguo unaondoka nalo, nategemea kwa kuwa hapa ni Makao Makuu kutakuwa na aina zote za magari yanayotengenezwa na Toyota,” Mhe. Senyamule

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Auto Garage action Bw. Saileshi Dattani, amewapongeza TEMESA Tanzania kwa kuwa amini na kuendelea kushirikiana nao hususani katika kutengeneza Magari ya Serikali.

Hata hivyo, uzinduzi wa Karakana hiyo umeambatana na uzinduzi wa Chumba Cha maonesho ya magari (Show room) pamoja na sherehe za kutimiza miaka 21 ya wamiliki wa karakana hiyo tangu walipotawazwa Uwakala wa Toyota Mwaka 2003.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *