TOVUTI ZA HALMASHAURI KUBORESHWA KUENDANA NA MABADILIKO

0

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali Bi. Nteghenjwa Hosseah amewatembelea wataalam wa Habari na Teknolojia ya habari kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Mradi wa Uboreshaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3+ – USAID) walioko mkoani Morogoro kwa ajili ya uboreshaji wa mfumo wa GWF unaosimamia Tovuti ya Ofisi ya Rais TAMiSEMi, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Wataalam hao wako kambini kwa ajili ya kufanya maboresho ya Mfumo huo wa GWF ambao ulianza kutumika mwaka 2017 na kuleta mafanikio makubwa katika utoaji wa habari za uhakika kwa wananchi.

Kufuatia mabadiliko ya Teknolojia katika siku za karibuni wataalam hao walitakiwa kuboresha Mfumo huo ili kuendena na kasi ya mabadiliko ya Teknolojia ya habari na kuendelea kuwa chanzo cha uhakika cha upatikanaji wa taarifa kwa wananchi.

Katika kikao hicho Bi. Hosseah amewataka wataalam hao kutumia nafasi hiyo kuhakikisha wanakamilisha uboreshaji wa mfumo wa GWF mapema ili uanze kutumika ili kukidhi malengo ya uanzishwaji wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *