SILINDE AIPONGEZA EQUITY BENKI KUTOA MIKOPO KWENYE ZAO LA KAHAWA

0

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) ameshiriki hafla ya utiaji saini Hati ya Makubaliano (Memorandum of Understanding) ya awali kwa ajili ya kutoa mikopo kwenye zao la Kahawa baina ya Benki ya Equity kwa kushirikiana na Mkoa wa Kagera, kupitia Halmashauri za Karagwe na Muleba leo Agost 5, 2024 katika Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa Nane Nane jijini Dodoma.

Makubaliano hayo yamelenga kuwafikia zaidi ya wakulima wadogo 4,000 ambapo Halamashauri hizo zimetenga zaidi ya ekari 4,000 kwa ajili ya Block Farming.

Kupitia makubaliano haya Halamashauri hizo zinatarajia kukopeshwa matrekta mawili kwa kila Halmashauri (New Holland, 75Hp) kwa ajili ya maandalizi ya mashamba haya ya Block Farming.

Mhe. Silinde amepongeza Benki ya Equity kwa uamuzi wake wa kuwasaidia wakulima katika Halmashauri hizo pamoja na kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita kuleta mageuzi katika Sekta ya Kilimo nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *