DIWANI CUP YAZINDULIWA KWA KISHINDO MAKOLE JIJINI DODOMA.

0

Uzinduzi wa Diwani Cup umefanyika Kata ya Makole Jijini Dodoma.

Mashindano hayo ya Mpira wa Miguu ambayo yanafadhiliwa na Diwani wa Kata ya Makole Mhe. Omary Omary yanashirikisha Timu Takribani 13 za Kata hiyo na Timu za Kata Jirani huku Bingwa akitarajiwa kuibuka na Zawadi nono.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi ambao umefanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Makole Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini Ndg. Amani Mulagizi amewaasa Vijana kushiriki michezo ili kujipatia Ajira lakini pia itawasaidia kuepukana na vitendo viovu kama Utumiaji wa madawa ya kulevya.

“tunatumia michezo kuwakutanisha kwaajili ya kubadilishana mawazo, lakini pia tunatumia michezo hii kuhamasisha baadhi ya mambo mbalimbali ikiwemo Mwaka huu ni mwaka wa Uchaguzi, kwahiyo tunategemea kutumia nafasi hii kuwahamasisha vijana wengi wajitokeze kugombea Katika nafasi za Serikali za Mitaa kwani Serikali na Chama Cha Mapinduzi inatoa fursa Kwa vijana kushika nyadhifa za Uongozi.

Naye Diwani wa Kata ya Makole Mhe. Omary Omary ambaye ndiye mfadhili wa mashindano hayo amesema lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Sekta ya Michezo katika kuhamasisha michezo na kuibua vipaji.

Ameeleza Bingwa wa Mashindano Mshindi wa Kwanza atapata mbuzi wawili, pamoja na set moja ya jezi, Mshindi wa Pili atapata Set moja ya Jezi pamoja na mbuzi mmoja, huku Mshindi wa Tatu akipata Jezi set moja.

Pia wakati wa Uzinduzi huo Timu zote shiriki zimekabidhiwa vifaa vya michezo ambavyo ni Jezi pamoja na Mipira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *