WAZIRI KUNDO ACHARUKA ATOA MAAGIZO MATANO KWA MKANDARASI WA MAJI WILAYA YA GEITA.
Naibu waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew amesekitishwa na mwenendo wa ujenzi wa mradi wa maji wa miji 28 unaojengwa katika kijiji cha Senga kata ya Senga Wilaya na Mkoa wa Geita kutokana na kusuasua kwa ujenzi wa mradi huo hali ambayo inapelekea mradi huo kuchelewa kukamilika na kusababisha wananchi kukosa huduma ya maji safi na salama katika maeneo yao.
Mhandisi Kundo amesema hayo leo Julai 20 2024, baada ya kufanya ukaguzi wa mradi huo unaogharimu bilioni 124 nakujionea maendeleo ya utekelezaji wa mradi ulioaanza kujengwa toka mwezi april, 2023 ukitarajiwa kukamilia 2025 lakini mpaka sasa upo asilimia 18 pekee na kumtaka Mkandarasi anayejenga mradi huo M/S AFCONS LIMITED kufanya kazi usiku na mchana pamoja na kuongeza wafanyakazi wa kutosha ili kuweza kukamilisha ujenzi wa mradi huo mapema.
Mhandisi Kundo amewaagiza Meneja wa RUWASA Mkoa wa Geita na Mkurugenzi wa GEUWASA kufanya ufuatiliaji wa ujenzi wa mradi huo mara kwa mara ili kumsimamia Mkandarasi huyo kumaliza mradi huo kwa wakati.