“KUENZI UTAMADUNI NI JAMBO LA MSINGI” – RC SENYAMULE

0

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa kufunga Tamasha la 15 la Muziki wa Cigogo lililofanyika katika Ofisi za viwanja vya Sanaa, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Julai 21, 2024.

Mhe. Senyamule amezungumza na makundi mbalimbali yaliyoshiriki Tamasha hilo na kusema kuwa kuenzi Utamanidu ni Jambo la Msingi kwani lilianza tangu enzi za waasisi wa Nchi.

“Utamaduni ni Utambulisho wetu inaweza kuwa mavazi, ngoma au vifaa. Hivyo tuendelee kutunza utamaduni wa kila Kabila kwa mtu mmoja mmoja na watanzania kwa ujumla”.

“Kila Wilaya ichukue nafasi yake ya kuiga utaratibu huu walioufanya Chamwino kwani ni Jambo zuri katika Mkoa kwa ujumla na tutafuta mshindi wa Kimkoa ili kila mahali suala la kukuza utamaduni lisiwe la hiyari bali liwe ni wajibu wa Kila Mtanzania”

Pia Mhe. Senyamule amesisitiza vikundi vyote vya ngoma vitumike kutoa Elimu kwa vijana na makundi mbalimbali juu ya kuimarisha maadili katika Jamii.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja, amesema utamaduni uliooneshwa katika Tamasha hilo upo katika vijiji 107 na hata ikitokea kikao cha kusikiliza kero au kusoma mapato ya Kijiji, watu waanze na utamaduni wa ngoma kuonesha jinsi unavyotunzwa na kurithishwa kizazi hadi kizazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *