“MADAKTARI FANYENI KAZI KWA BIDII, UPENDO NA HURUMA” MBUNGE TAUHIDA
Madaktari wa Kituo cha Afya KVZ Mtoni wametakiwa kufanya kazi kwa bidii, upendo na huruma ili kujenga Imani na wateja wao.
Mbunge wa viti Maalum Mhe. Tauhida Galls amesisitiza hayo katika Hospitali ya KVZ Mtoni Mara baada ya kukabidhi Vifaa mbalimbali ikiwemo Mashuka na Sabuni katika Hospitali hiyo.
Amesema Wananchi wanajenga Imani ya kutibiwa katika Kituo hicho kutokana na kuwepo nidhamu na ukarimu kwa Wateja wao wanapokwenda kupata huduma.
Aidha Mhe. Tauhida amesema kituo hicho kina mchango mkubwa kwa jamii hivyo ameahidi kukiunga mkono kwa hali na mali ili kuzidi kutoa huduma bora kwa Askari wake, Familia na jamii kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkuu wa Kkosi cha KVZ Luteni Kanali Said Shamuhuna amesema Kituo hicho kilianza kutoa hutuma kwa askari na familia zao lakini kwa sasa wanapokea wajongwa kutoka maeneo mbalimbali katika jamii.
Hivyo katika mwaka wa fedha 2024-2025 wanakusudia kujenga Hospitali kubwa ya Ghorofa moja kwa Unguja na nyingine kisiwani Pemba ili kutoa huduma kwa Wagonjwa wengi zaidi.
Nae Mkuu wa Kituo Cha Afya KVZ Mtoni Meja Shemsha Bakari Kusupa amesema msaada huo umekuja kwa wakati muafaka na kuahidi kuufanyia kazi kama ilivyokusudiwa.
Hata hivyo amewaomba Wafadhili na Watu wenye uwezo kujitokeza kutoa misaada yao ili kufikia malengo yaliopangwa na Kituo hicho.