MWENGE WA UHURU KUKAGUA MIRADI 57 YA MKOA WA MANYARA

0

Na Mary Margwe, Hanang

Mwenge wa uhuru umetua Mkoa wa Manyara ukitokea Mkoa wa Singida, ukiwa katika Mkoa Manyara utatembelea jumla ya miradi 57 yenye thamani ya sh.bil.149.5.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Queen Cuthbert Sendiga mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Godfrey Eliakimu Mnzava , Mkuu wa Mkoa wa Sindida Halima Omary Dendego, wakati alipokua akitoa salamu wakati wa mapokezi ya Mwenge wa uhuru katika Kijiji cha Gehandu Wilayani Hanang Mkoani humo.

Sendiga amesema Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Manyara utakimbizwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa 7 ambazo Hanang, Mbulu Wilaya, Mbulu Mji, Babati Wilaya, Babati Mji, Kiteto na Simanjiro Kwa mzunguko wa kilometa 980.5, ukiwa Mkoa hapa Mwenge wa uhuru utatembelea miradi 57 yenye thamani ya sh.bil.149.5

Aidha Mwenge wa uhuru Mwaka 2024 ukiwa Mkoani hapa utafanya kazi ya kuweka mawenya msingi miradi 17 yenye thamani ya bil.134.1, kuzindua miradi 8 yenye thamani ya bil.3.4, Kufungua miradi 4 yenye thamani ya sh.bil.1.3 na kukagua miradi / kuona miradi 28 yenye thamani ya sh. Bil.10.7

” Mchangnuo katika uchangiaji wa miradi hii ni kama ifuatavyo, nguvu za wananchi sh. Mil. 102.5, Serikali Kuu sh.bil.72.8, Halmashauri sh.mil.169.7 huku wadau wengine wakichangia sh. Bil.76.5 ” amesema Queen Sendiga.

Aidha Mkuu wa Mkoa huyo aliwashukuru wananchi wa Mkoa huo kwa kuibua, kuanzisha , kuchangia na kuitekeleza miradi hiyo, huku aliwashukuru wadau wa maendeleo ambao wameweza kuchangia shughuli za Maendeleo katika Mkoa huo.

” Nitumie fursa hii kuwashukuru wananchi wa Mkoa huu kwa kuibua, kuanzisha , kuchangia na kuitekeleza miradi hiyo, huku aliwashukuru wadau wa maendeleo ambao wameweza kuchangia shughuli za Maendeleo katika Mkoa wetu” amesema Sendiga.

” Tunafahamu mbio za Mwenge wa uhuru Kwa mwaka 2024 ni mbio Maalum kwani zinatimiza miaka 60 yangu zilipoanza, lakini pia imetimia miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na vilevile imetimia miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yangu ilivyoasisiwa na viongozi wetu Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Kalume ( Mungu azilaze roho zao Mahali pema peponi)” amesema Sendiga Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Hata hivyo Mkuu huyo amefafanua kuwa pamoja na jumbe zingine za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2024, Mkoa wa Manyara umejiandaakuupokea ujumbe mahususiwa Mwenge wa uhuru wa Mwaka 2024 unaosema ” Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *