SHULE MPYA YA SEKONDARI KUJENGWA KATA YA CHIHANGA-MAVUNDE

0

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amewahakikishia wananchi wa kata ya Chihanga kwamba Serikali ya awamu ya sita chini ya Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ili kupunguza changamoto mbalimbali zinazoikabili kata hiyo ikiwemo ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari ili kuwapunguzia mwendo wanafunzi ambao kwa sasa wanaifuata shule ya Sekondari iliyopo kwa kutembea umbali mrefu.

Mbunge Mavunde ameyasema hayo wakati wa mkutano wa wananchi wa kata ya Chihanga ambao pamoja na kusikiliza changamoto za wananchi lakini pia kupokea taarifa ya wenyeviti wa mitaa wanaomaliza muda wao.

“Tunaishukuru Serikali kwa utekelezaji mkubwa wa miradi ya umeme,elimu,afya na maji.

Utekelezaji wa mradi wa umeme ndani ya kata umechochea kwa kiwango kikubwa shughuli za kiuchumi na kuwezesha wananchi wengi kujiajiri.

Moja ya changamoto kubwa iliyopo kwa sasa ni upatikanaji wa shule mpya ya Sekondari katika eneo la Chamwino ili wanafunzi wanaotoka maeneo mbalimbali ndani ya kata ya Chihanga waweze kuifikia kwa urahisi,ninaahidi kupitia Mfuko wa Jimbo kujenga darasa 1 kuanzisha ujenzi huo kabla ya serikali haijatuunga mkono kwenye ujenzi huu.

Tumetenga zaidi ya Tsh 50m kumalizia ujenzi wa Zahanati ya Sogeambele na RUWASA imeanza kuipitia na kuirekebisha miradi yote yenye changamoto ya upatikanaji wa Maji sambamba na ukarabati wa miundombinu ya Barabara”Alisema Mavunde

Akizungumza katika mkutano huo Diwani wa kata ya Chihanga Mh. Allice Kitendya amemshukuru Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa ujenzi wa madarasa 8,mradi mkubwa wa usambazaji wa umeme ambayo ilikuwa ni kero kubwa sana na pia kutumia fursa hiyo kumshukuru Mbunge Mavunde kwa kuunga mkono shughuli za maendeleo ndani ya kata hiyo ikiwemo uanzishwaji wa ujenzi wa Zahanati ya Sogeambele,Mchango wa Tsh 2,500,000 kwa ajili ya Ununuzi wa ardhi ya matumizi ya huduma za kijamii,Matofali 2000 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi na ahadi ya ujenzi wa darasa la Shule Mpya ya Sekondari eneo la Chamwino.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *