MIFUMO IMESAIDIA KULETA UWAZI, UWAJIBIKAJI NA UDHIBITI WA MATUMIZI YA FEDHA

0

Naibu katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI (Elimu) Dkt Charles Msonde amesema Mifumo mbalimbali inayoanzishawa na Serikali imekuwa na mchango mkubwa katika kuleta Uwazi, Uwajibikaji na Udhibiti wa matumizi ya Fedha za umma na kusaidia katika upangaji wa Bajeti na utoaji wa taarifa kwa uwazi.

Dkt.Msonde amesema hayo leo Julai 10, 2024 wakati akifungua wa Mkutano wa Upangaji Mipango Pamoja wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za umma Awamu ya Pili yaani USAID public sector systems strengthening plus (USAID PS3+) uliofanyika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jengo la Mkapa Jijini Dodoma.

Amesema Mradi wa PS3+ Umeshirikiana na Serikali katika usimamizi na utoaji wa huduma mbalimbali, akitolea mfano huduma za Mifumo inayoanzishwa ili kurahisisha shughuli za Serikali ambazo zimewezesha wananchi kupata huduma mbalimbali kama vile za Afya na Elimu.

Ametaja baadhi ya mifumo kuwa ni mfumo wa Kihasibu na Utoaji wa Taarifa za Fedha katika Ngazi za Msingi (FacilityFinancial Accounting and Reporting System – FFARS) ambao umewezeshwa kutumika katika ngazi ya shule za Sekondari na Msingi, vituo vya kutolea Huduma za afya, Kata, Vijiji na Mitaa ili kuleta uwazi, uwajibikaji na kudhibiti matumizi ya fedha katika ngazi za msingi za Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mfumo wa uandaaji mipango na bajeti(PlanRep), Mfumo wa Ukusanyaji Mapato -TAUSI, Mufumo wa Ulipaji Serikalini -MUSE pamoja na Tovuti za Mikoa and Halmashauri (GWF).

Aidha Dkt Msonde amewaelekeza wajumbe wa mkutano huo kutumia kutumia fursa hii muhimu kwaajili ya kuangalia mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa Mradi huu  na kuzitatua changamoto hizo ili kuweza kufanikisha mradi huu na kuwatumikia wananchi.

Pia ameagiza kuwe na ushirikishwaji wa wananchi katika matumizi ya mifumo hiyo kwaajili ya maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Naye Mkuu wa Timu ya Uboreshaji Mifumo kutoka Shirika la USAID Tanzania Bw. Godfrey Nyombi, amesema kuwa Mifumo hii inatumika kwa shughuli za kila siku kama vile usimamizi wa fedha, Mipango, taarifa, mawasiliano kwa wananchi na inasomana na mifumo mingine hivyo kurahisisha shughuli za kimaendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *