NAIBU WAZIRI MKUU AZINDUA TOVUTI RASMI YA MAONESHO YA NANENANE 2024
Tovuti rasmi ya Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa ya Nane Nane 2024 imezinduliwa na Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko (Mb), Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati leo tarehe 6 Julai 2024, mkoani Tabora wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani (SUD 2024). Uzinduzi huo umeshuhudiwa na Mhe. Hussein Bashe (Mb), Waziri wa Kilimo.
Wizara ya Kilimo inawakaribisha Wakulima, Wafugaji, Wavuvi, Wafanyabiashara, Wawekezaji, Wazalishaji, Taasisi za Fedha na Wadau wote wa ndani na nje ya nchi kwenye mnyororo wa thamani katika Sekta ya Kilimo kushiriki maonesho hayo ambayo yanatoa fursa za kibiashara na za kujifunza teknolojia za kisasa kwenye kilimo.
Kauli mbiu ya Nanenane Mwaka 2024 ni “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.
Ili kupata nafasi ya banda la Maonesho tafadhali tembelea https://nanenane.kilimo.go.tz au piga simu namba 0712 310648 au Namba 0658 860870.