SPIKA DKT. TULIA KATIKA MKUTANO WA JUKWAA LA KIBUNGE LA JUMUIJA YA MAENDELEO YA KUSINI MWA AFRIKA (SADC-PF)

0

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akifuatilia Mkutano wa Jukwaa la Kibunge la Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-PF) unaoendelea leo tarehe 4 Julai, 2024 Luanda nchini Angola.

Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo utajadili na kuweka maazimio ya Dhima kuu ya Mkutano huo ambayo ni “Nafasi ya Mabunge kuwa chachu ya matumizi ya Nishati mbadala na safi kwa maendeleo endelevu ya Jumuiya ya Kusini mwa Afrika.”

Katika Mkutano huo, Dkt. Tulia ameambatana na Wabunge Wawakilishi kutoka Tanzania akiwemo Mhe. Selemani Zedi, Mhe. Shally Raymond, Mhe. Hawa Mwaifunga, Mhe. Dkt. Alfred Kimea na Mhe. Kassim Haji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *