WANAUME WATAKIWA KUTOA TAARIFA WANAPOFANYIWA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA

0

Mkuu  wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Sigida,Thomas Apson, amewataka wanaume kutoa taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia wanavyofanyiwa, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kabla mambo hayajaharibika.


Mkuu huyo wa Wilaya ametoa wito huo juzi, wakati akizundua jengo la Dawati la ukatili wa kijinsia lililopo kwenye eneo la ofisi ya polisi wilaya ya Ikungi.

Amefafanua kuwa uzoefu unaonyesha wanaume wengi wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia  na wake zao au marafiki zao wa kiume,lakini huwa hawatoi taarifa.

“Wanakaa kimya wala hawatoi taarifa.Hilo ndilo tatizo kubwa.Ukimya huo unachangia vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsi viwe  sugu, na vinasababisha madhara makubwa. Ikiwemo kuvunjika kwa ndoa au kusabababisha vifo”,alisema.

Kuhusu Dawati, amesema kuwa serikali ikishirikiana na shirika la KOICA na mwakilishi Farm Africa,wamejenga jendo hilo la Dawati kwa shilingi milioni mia moja.

“Jengo hili ni rafiki kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinjisia.Lina vyumba vya faragha ambavyo mhanga atajieleza kwa uhuru mpana.Yote yatakayozungumzwa,yatakuwa ni siri ya mtoaji malalamiko na mpokeaji.Kikubwa zaidi,naomba nitumie nafasi hii,kuomba vyombo vya humu ndani ,vitunzwe ili ziweze kutumika kwa muda mrefu”,Apson amesisitiza.

Kwa upande wake Naibu mwakilishi mkazi wa UN Women Tanzania Katherine Gifford,amesema moja ya hatua madhubuti walizochukua,ni kuunga mkono juhudi za  serikali katika kutetea waathirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia, ndani ya jamii.

Pia alisema  waliwekaza  umuhimu mkubwa katika safari yao ya pamoja ya  kuelekea kwenye usawa wa kijinzia na kuwawezesha wanawake kiuchumi nchini Tanzanaia.

“Katika kipindi cha miaka minne iliyopita,UN Women kwa ufadhili wa shirika la maendeleo la Korea,(KOICA),tumeongeza kupigia chapuo jitihada za kuleta usawa wa kijinzia kwa kuwawezesha wanawake na wasichana balehe.Umuhimu mkumbwa ulielekezwa  katika halmashauri za Msalala na Kahama mkoani Shinyanga,na Ikungi mkoani Singida”,amesema.

Katherine alisema kuwa jitihada hizo za pamoja, zimekuwa muhimu mno katika kusukuma mbele matamanio yao ya pamoja. Ambayo ni kuleta usawa wa kijinzia na kupunguza umaskini,Kwa kuzingatia sera ya Taifa.

Awali mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ikungi,Justin Kijazi,amesema kuwa wakishirikana na shirika la UN Women,wametelekeza miradi mbali mbali ya uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.

Ametaja baadhi ya miradi hiyo, kuwa ni mradi wa kufikia usawa wa kijinsia kwa kuwezesha wanawake na wasichana kiuchumi.Na mradi wa ushiriki wa wanawake na walemavu, kwenye uongozi.

“Miradi hii na mingine mingi,imegusa kata saba na vijiji 18 kwa lengo la kuleta usawa katika kufikia maendeleo, bila kumwacha nyuma mwana jamii ye yote.Mafanikio yaliyofikiwa na mradi uliokamilika, na hii inayoendelea,ni pamoja na kuongeza kipato kwa wanawake kwa asilimia 22”,amesema.

Mkurugenzi Kijazi,ametumia nafasi hiyo kushukuru shirika la UN Women kwa kutimiza ahadi yao kwa halmashauri hiyo ya Ikungi.Hivyo wameombwa  waendelee kufadhili miradi mbali mbali ya maendeleo.

Katika hatua nyingine,Kijazi ametangaza kwamba wanaendelea kumalizia ujenzi  wa hospitali ya wilaya hiyo ya Ikungi.Hospitali hiyo ni ya kiwango cha juu.Itawapunguzia wananchi kufuata huduma za matibabu, umbali mrefu.

Naye katibu CCM wilaya ya Ikungi,Joshua Hungura Mbwana,amesema katika ziara yake ya hivi karibuni,ameridhishwa na jinsi miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na uongozi wa halmashauri.Miradi hiyo ina thamani ya fedha zilizotumika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *