VIJANA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI ZINAZOPATIKANA HALMASHAURI.
Mtandao wa Vijana wa TK Movement ambalo linajishughulisha kuendeleza vuruvugu la kujitolea ili kuleta mapinduzi ya kitaifa limewataka vijana nchini kuchangamkia fursa zilizopo kwenye halimashauri ili mujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Mratibu wa TK Movement, Sophia Jumbe,alitoa wito huo wakati akizungumza na viongozi wa vijana wa mtandao huo katika halmashauri za Wilaya ya Manyoni na Itigi mkoani Singida.
Sophia katika ziara hiyo aliambatana na Kamati ya Uratibu ya Mkoa ya mtandai huo,akiwemo Mratibu Msaidizi Simtemvu Sitambuli, Katibu Mkoa wa Mtandao,Ibrahim Wawa na Mkuu wa Idara ya Makundi Muhimu, Ahmedi Misanga.
Amesema vijana ni kundi muhimu sana katika harakati za kukuza uchumi wa nchi hivyo ili kufikia malengo hayo vijana wanapaswa kuchangamkia fursa za mikopo,ajira na uongozi.
“Vijana wezangu na viongozi wa Tk Movement ebu tutumie furusa zipo kwenye nchi yetu mnaa mama yetu amefanya kazi kubuwa katika sekta zote hivyo twendeni tukatumie fursa hizo,”alisema.
Aidha, Sophia aliwataka viongozi hao kujipanga na kuendelea kutoa hamasa kwa jamii ili kuelewa kazi na majukumu ya TK Movement kwa vijana wa Mkoa Singida.
Ameongeza kuwa Julai 18,2024 kutakuwa na tukio la uzinduzi wa Tk Movement katika Mkoa wa Singida
hivyo tufanye hamasa ya kutosha ili vijana waje kwa wingi kujifunza na kujua fursa zipo.
Naye Mkuu wa Idara ya Makundi Muhimu,Ahmedi Misanga awaliwaasa vijana kujitoa na kujituma kwenye taifa lao.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi,Hussein Simba, amesema halmashauri itakuwa tayari kushirikiana na mtandao wa TK ili kuona namna vijana wanapata fursa mbalimbali zinazopatika katika halmashauri hiyo.
“Napenda kuishukuru Serikali ya awamu ya sita
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
kwa kuweka mazingira mazuri kwa vijana wa TK Movement wezangu twende tukayaseme mambo hayo mazuri kwenye makundi yote tuliyonayo,”amesema Misanga.
Kwa upande wake katibu wa Tk Movement Mkoa wa Singida, Ibrahim Wawa aliwakumbusha viongozi wa myandao huo kufuata misingi ya kujitole,kujituma na kuchangamkia fursa zilipo hapa Nchini.
“TK MOVEMENTS NI MTANDAO WA VIJANA NA WANAWAKE WENYE LENGO LA KUENDESHA VUGUVUGU LA KUJITOLEA ILI KULETA MAPINDUZI YA KIFIKRA KWA JAMII NA KUHIMIZA USHIRIKI KWENYE FURSA UBORA WA MTANDAO HUU NI KWAMBA HAFUNGAMANI NA UPANDE WOWOTE WA KISIASA KIDINI KABILA AMA UTAMADUNI,