SERIKALI YAANZA UJENZI TUTA MTO LUMEMO

0

Serikali imeanza mchakato wa kukabiliana na Mafuriko katika Mji wa Ifakara Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro Kwa kijenga tuta tuta kubwa mto lumemo baada ya mvua za masika kuleta madhara makubwa kuvunja kingo za mto huo maji kuimgia kwenye makazi ya watu

Mhandisi wa bodi ya Maji Bonde la Rufiji Emanuel Lawi amesema ujenzi wa tuta hilo utagharimu milioni mia nne na litakua na urefu wa Kilometa 12 na sasa tayari Umefikia asilimia 40

Mkuu wa wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya amesema ujenzi wa tuta hilo ni njia ya kuokoa upotevu wa maji ya mto huo Lumemo na kuyaelekeza katika mto Kilombero ambao unachangia asilimia 65 ya maji kwenye bwawa la Mwalimu Nyerere.

Kamanda wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji wilaya ya Kilombero Mkaguzi wa Zimamoto Haji Madulika amesema mvua za masika zimeleta athari kubwa katika eneo hilo Kwa kusababisha vifo ,nyumba kubomoka na Mazao kusombwa huku wananchi wakipongeza ujenzi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *