SPIKA DKT. TULIA AWASILI LUANDA NCHINI ANGOLA

0

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 1 Julai, 2024 amewasili Luanda Nchini Angola na kupokelewa na Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini humo Mhe. Mbwana Mziray.

Dkt. Tulia anatarajia kushiriki Mkutano wa 55 wa Jukwaa la Kibunge la Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-PF) unaoanza rasmi kesho tarehe 2 na kuhitimishwa tarehe 6 Julai, 2024. Mkutano huo umebeba Ujumbe wa nafasi ya Mabunge kuwa chachu ya matumizi ya Nishati Mbadala na safi kwa maendeleo endelevu ya Jumuiya ya Kusini mwa Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *