DC AWAMBOGO ATOA SIKU TISA ZAHANATI ILIYOKAMILI MIAKA 3 IANZE KUFANYA KAZI

0

Mkuu wa wilaya wa Geita Hashim Komba ameiagiza halmashauri ya mji Geita kuhakikisha adi kufika tarehe 10 mwezi wa saba zahanati iliyokamilika mwaka 2022 iliyopo katika kijiji cha ibanda iwe imefunguliwa na wananchi wa kijiji hicho waondokane na adha ya kufata huduma ya afya umbali wa kilomita 15.

Ameyasema hayo katika ziata yake ya kukagua miradi iliyokwamba katika halmashauri ya mji Geita na kukuta zahanati hiyo haitoi huduma ikiwa imeshakamilika kwa kila kitu ikiwemo choo, kichomea taka pamoja na thamani za ndani huku jingo hilo likiendelea kuchakaa na kuharibika baadhi ya maeneo.

Diwana wa kata ya kanyala Barnabas Mapande iliyopo katika halmashauri ya mji Geita amesema ujio wa mkuu wa wilaya katika kata hiyo kutasaidia kwa kiwango kikubwa kutatua changamoto mbalimbali zinazo wakabili wananchi hao ikiwemo zahanati hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *