MADIWANI WAIPONGEZA TANESCO KINONDONI KUSINI KWA KUTOA HUDUMA BORA

0

Na. Noel Rukanuga – DSM.

Madiwani wa Manispaa ya Ubungo na Kinondoni wameipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kinondoni Kusini kwa kutoa huduma bora kwa wananchi katika mkoa huo kwa kuwasikiliza na kutatua changamoto za huduma za umeme kwa wakati.

Akizungumza leo Juni 28, 2024 katika Ukumbi wa Shule ya Sheria (School of Law) katika kikao kazi cha kujadili Maendeleo ya Sekta ya Umeme  kilichowakutanisha Madiwani wa Manispaa ya Ubungo na Kinondoni pamoja na Menejimenti ya TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kusini, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Mhe. Jaffary Juma Nyaigesha, amesema kuwa tanesco wamekuwa wapo karibu na wananchi jambo ambalo limesaidia kufanya kazi kwa ufanisi.

Mhe. Nyaigesha amesema kuwa kila wakati madiwani wa Manispaa ya Ubungo na Kinondoni wamekuwa wakishirikishwa na TANESCO kuhusu utekelezwaji wa masuala mbalimbali ya miradi ya umeme  jambo ambalo limeleta tija katika utendaji wa madiwani  hasa kutoa taarifa au ufafanuzi kwa wananchi kuhusu huduma za tanesco katika mkoa wa Kinondoni Kusini.

“Ushirikiano wa TANESCO na madiwani ni mkubwa na unaleta ufanisi katika kazi kwani linapotokea kero ya huduma ya umeme kwa wananchi linatatuliwa kwa wakati” amesema Mhe. Nyaigesha.

Mhe. Nyaigesha amesema kuwa kupitia kikoa hicho madiwani wapewa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ikiwemo athari za uhalibifu wa miundombinu ya umeme, maboresho ya mita, utaratibu mpya wa kuomba huduma ya umeme kupitia mtandao (online), maendeleo ya mradi wa kuzalisha umeme wa Bwawa la  Julius Nyerere pamoja na Wizara ya Nishati na Madini.

“Tunampongeza Rais Dkt. Samia Suruhu Hassani kwa kuendelea kufanya uwekezaji mkubwa kwa kuboresha miundombinu pamoja kuanzisha miradi mpya ya kuzalisha umeme ili wananchi waweze kupata huduma bora” amesema  Mhe. Nyaigesha.

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kusini Mhandisi Florence Mwakasege, amesema kuwa wanaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali katika mkoa huo pamoja na kuboresha miundombinu ya umeme ili kuleta tija kwa Shirika na Taifa katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

Mhandisi Mwakasege ametoa wito kwa madiwani kuendelea kutoa ushirikiano wa kufikisha taarifa kwa wananchi kuhusu masuala ya huduma ya umeme katika mkoa huo kupitia vikao vyao.

“Kupitia kikao kazi hiki kitasaidia kubaini changamoto zilizopo kwenye kata tunazo hudumia  ili tunapokwenda kuandaa mpango kazi kwa mwaka wafedha mpya tuweze kuzitatua kwa haraka ” Mhandisi Mwakasege.

Katika kikao kazi hicho walishiriki viongozi mbalilmbali akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ubungo, Menejimenti ya TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kusini pamoja na  Wilaya ya Ubungo na Kinondoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *