DC MTAMBULE AGAWA MITUNGI YA TAIFA GAS KWA WANACHUO, BODABODA NA AKINA MAMA

0

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule amezindua Duka la Kampuni ya Taifa Gas lililopo eneo la Changanyikeni, Kata ya Makongo mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza jana Juni 27,2024 katika hafla ya uzinduzi huo ulioambatana na ugawaji wa mitungi ya gesi 100 kwa wanafunzi wa vyuo vikuu yaani Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Takwimu na Chuo cha Maji, bodaboda na akina mama, Mtambule aliipongeza Kampuni ya Taifa Gas kwa kuunga mkono kwa vitendo kampeni ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhamasisha matumiza ya nishati safi ya kupikia.

“Tangu mwaka 2022 tumeona jinsi Rais Dkt. Samia alivyo mstari wa mbele katika kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, na hili linajidhihirisha mwaka huu ambapo Rais alikwenda pia nchini Ufaransa kweny mkutano mkubwa wa masuala ya nishati safi ya kupikia na tuliona jinsi alivyohamasisha jambo hili. Hivyo hiki mnachokifanya Taifa Gas ni mwendelezo wa Kampeni hiyo,” alisema Mtambule.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule akizindua Duka la Kampuni ya Taifa Gas lililopo eneo la Changanyikeni, Kata ya Makongo mkoani Dar es Salaam, Tarehe 26 Juni 2024.

Mtambule alibainisha kuwa matumizi ya nishati isiyo safi ya kupikia yaani kuni na mkaa vinaathari kwa mazingira na afya kwa binadamu, kwamba zaidi ya watu 30,000 kwa mwaka wanafariki kutokana na athari ya matumizi ya nishati isiyo safi ya kupikia.

Hivyo alieleza kuwa ni muhimu kwa sasa kuongeza idadi kubwa ya wananchi wanaotumia nishati safi ya kupikia kwa ajili ya kulinda mazingira pamoja na afya zao, ambapo alibainisha kuwa kwa sasa ni asilimia 10 tu ya wananchi ndio wanatumia nishati safi ya kupikia.

“Nawapongeza Taifa Gas kwa mwitikio huu wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia. Tunashukuru kwa namna mlivyoyapokea maono ya Rais Dkt. Samia na kuyatekeleza. Hili ni jambo la kuwapongeza sana,” alisisitiza Mtambule.

Mtambule alitumia fursa hiyo kuwahimiza wanafunzi hao pamoja na wananchi kwa ujumla kutumia nishati safi ya kupikia na kuwataka kuhamasisha na watu wengine kwani nishati isio safi ya kupikia ina madhara makubwa kwa mazingira na afya.

Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Taifa Gas Joseph Nzumbi alisema kuwa kwa wanafunzi waliowapatia mitungi hiyo wanapaswa kujisajili kwenye program (App) ya Taifa Gas ambapo itawawezesha kujaza gesi kwa bei ya punguzo kwamba wa mtungi wa kujaza kwa shilingi 23,000 wataweza kujaziwa kwa shilingi 20,000 huku kwa mtungi wa shilingi 55,000 wakijaziwa kwa shilingi 50,000.

“Kama Taifa Gas tunaendelea kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia, tunataka asilimia 80 ya wananchi watumie gesi. Tunaamini kwa kiasi hiki kidogo tulichogawa leo (jana) tutakuwa tumepunguza idadai ya watumiaji wa nishati isio safi ya kupikia,” alisema Nzumbi.

Awali Meneja Mahusiano wa Taifa Gas Angela Bhoke alisema kuwa wanagawa mitungi 100 kwa makundi matatu yaani wanafunzi kutoka vyuo jirani na Changanyikeni ambavyo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Takwimu na Chuo cha Maji.

Alibainisha kuwa mitungi hiyo 100 waliyogawa yenye thamani ya shilingi milioni 22 ni ya awamu ya kwanza tu, kwani lengo ni kugawa jumla ya mitungi 300 na kwamba wamelenga kugawia wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wa pili.

Akizungumzia kuhusu uzinduzi wa duka hilo, alieleza kuwa wamefanya hivyo ikiwa ni mwitikio wa wito wa Rais Dkt. Samia wa kumtua mama mzigo wa kuni kichwani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *