BODI YA WAKURUGENZI NHC YAFANYA ZIARA MIRADI YA DAR

0

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) imefanya ziara katika miradi mbalimbali ya Shirika hilo iliyopo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi. Ziara hiyo iliyofanyika leo, ilianza saa nne asubuhi na kuwajumuisha wajumbe wote wa Bodi pamoja na viongozi waandamizi wa Shirika.

Katika ziara hiyo, Bodi ilipata fursa ya kutembelea miradi ya Kawe 711, Morocco Square, Samia Housing  na eneo la NHC Urafiki ambayo inajumuisha ujenzi wa nyumba za makazi na biashara. Mwenyekiti wa Bodi, Dk Sophia Kongela, alitoa maelekezo akitaka umuhimu wa kuimarisha utekelezaji wa miradi na kuhakikisha ubora unaendelea kuzingatiwa kwa kila hatua.

“Ni muhimu kwa Bodi yetu kufanya ziara kama hizi ili kujionea moja kwa moja maendeleo ya miradi yetu. Tunajivunia juhudi zinazofanywa na timu yetu ya ujenzi na tunahakikisha kwamba miradi yote inatekelezwa kwa viwango vya kimataifa,” alisema Dk.Kongela.

Viongozi wa NHC waliokuwepo katika ziara hiyo waliweza kutoa maelezo ya kina kuhusu changamoto zinazojitokeza katika ujenzi na hatua ambazo zimechukuliwa ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotarajiwa.

Bodi inaendelea  na  ziara katika miradi ya Samia, Morocco Square na Eneo la NHC Urafiki kufuatilia utekelezaji wa maelekezo na miongozo yake.

Ziara hii ni sehemu ya juhudi za NHC katika kuhakikisha kuwa inatoa suluhisho la makazi bora kwa wananchi na kusimamia rasilimali za umma kwa ufanisi na uwazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *