AWESO ATEMBELEA VIWANDA VYA KUZALISHA MITA ZA MAJI ZA MALIPO KABLA CHINA

0

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amehitisha ratiba ya ziara ya kikazi ya kimkakati nchini China kwa kutembelea viwanda mbalimbali vya kutengeneza na kuzalisha Mita za Maji za Malipo (PRE-PAID WATER METERS) kabla ili kujionea teknolojia mbalimbali katika kutengeneza mita hizo.

Waziri Aweso ameambatana na timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Maji ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara Mhandisi Mwajuma Waziri, Kitengo cha Manunuzi, Idara ya Usamabaziji maji na usafi wa Mazingira, Kitengo cha Sera na Mipango, Mhandisi wa Maji, Mkaguzi wa ndani, na wataalamu wengine.

Akifafanua mkakati wa Wizara ya Maji Waziri Aweso amesema Timu hii baada ya kujionea uzalishaji na aina mbalimbali ya Mita hizi , itaungana na Kamati maalum aliounda Wizarani na kwa pamoja zitakuja na muongozo wa namna gani utekelezaji wa mabadiliko haya utakavyofanyika hatua kwa hatua.

Aidha, Aweso akiwa katika ziara hii amesema ni wakati sahihi wa kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan juu ya kuelekea kwenye mabadiliko ya Mita za Maji kutoka zile za kawaida na kuanza kutumia mita za kisasa za Malipo kabla na kusisitiza kwamba wakati wa mabadiliko ni sasa.

Akihitimisha ziara yake viwandani Ningbo na Dhangai China, Mhe Aweso amesema pamoja na uhitaji wa mageuzi haya lakini upo umuhimu wa kujiridhisha na kufanya utafiti wa kutosha juu ya mita sahihi kwaajili ya matumizi ya nchi yetu zitakazozingatia ubora, uzalishaji toshelevu, uendelevu na thamani ya fedha ili zisiwe changamoto kwa wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *