AWESO ATEMBELEA GRID YA MAJI YA TAIFA NCHINI CHINA

0


Katika sehemu ya kushiriki Kongamano la Kumi na Tano la Ujenzi na Uwekezaji katika Miundombinu (15th International Infrastructure Investment and Construction Forum and Expo), Waziri Aweso ametembelea Gridi ya Maji ya Taifa ya China (South-to-North Water Diversion Project). Madhumuni ya kutembelea mradi huo ni kuongeza weledi katika maandalizi ya ujenzi wa Gridi ya Maji ya Taifa nchini Tanzania inayolenga kutumia vyanzo vikuu ya maziwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa na mito mikubwa kama Rufiji kusambaza maji maeneo mengi nchini yenye maji kidogo.

Gridi ya Maji ya Taifa ya China ina njia kuu tatu ambazo ni Mashariki, Kati na Magharibi zenye jumla ya urefu wa kilometa 4,350. Wakati sehemu ya Magharabi ya Gridi hiyo iko katika hatua za awali (planning), njia ya Mashariki (kilometa 1,466) na njia ya Kati (kilometa 1,432) zimekamilika. Njia hizo kwa pamoja zinalisha watu zaidi ya milioni 140 katika miji mikubwa na midogo zaidi ya 40 pamoja na majimbo na wilaya zaidi ya 280 katika maeneo ya Beijing na Tianjin miongoni mwa maeneo mengine nchini China.

Ziara katika mradi huu mkubwa dunia ni fursa kwa Tanzania katika kuboresha ujenzi wa Gridi ya Maji ya Taifa kwa matumizi ya sasa na vizazi vijavyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *