WAFANYAKAZI TUZINGATIE USALAMA KWANZA KAZINI – MHANDISI MWAKASEGE

0

Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kinondoni Kusini wametakiwa kuzingatie usalama kwanza wakati wanatimiza majukumu yao wakiwa mahala pakazi.

Akizungumza Juni 22, 2024 wakati akifungua Bonanza la Usalama na Afya
lililofanyika Viwanja vya michezo vya Shule ya Sheria Jijini Dar Dar es Salaam, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kusini Mhandisi Florence Mwakasege, amesema kuwa ni muhumi wafanyakazi kuzingatia usalama na afya ya mwili ili kuhakikisha wanakuwa vizuri muda wote na kuleta tija katika utendaji.

Mhandisi Mwakasege amesema kuwa michezo ni afya, hivyo wakati umefika kwa kila mtumishi ikiwemo kada ya madereva kutenga muda kwa ajili ya kufanya mazoezi kwani yana umuhimu mkubwa.

“Usikae muda mrefu bila kufanya mazoezi, mwili wa binadamu unatakiwa kuujenga na kuulinda kwa kuheshimu utaratibu wa kula chakula” amesema Mhandisi Mwakasege.

Aidha, Wafanyakazi walipata fursa ya kupata elimu kuhusu jinsi ya kujilinda na ajali eneo la kazi kutoka kwa Wakala wa Usalama wa Afya Mahali pa Kazi (OSHA).

Wafanyakazi kwa ujumla wameshukuru uongozi wa mkoa kwa kuanda Bonanza hilo kwani ni muhimu kwa afya zao.

Bonanza hilo liliongozwa na kauli mbiu isemayo ‘USALAMA KWANZA” ambapo wafanyakazi wamepata fursa ya kushiriki michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu kwa wanaume, mpira wa pete kwa wanawake, kuvuta kamba, bao, kukimbiza kuku, karata, pamoja na kukimbia na magunia.

Pia Bonanza lilikuwa na lengo la kutoa elimu kuhusu usalama mahala pakazi pamoja na kuimarisha afya na kuendeleza utamaduni wa kufanya mazoezi ili kuongeza ufanisi katika utendaji wakiwa katika umoja na mshikamano jambo ambalo litasaidia leta tija kwa Shirika na Taifa.

•Imeandaliwa na Noel Rukanuga kutoka Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *