NYONGO APONGEZA UONGOZI WA WILAYA YA MASWA

0

Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, Mhe. Stanslaus Nyongo amepongeza uongozi Wilaya ya Maswa kwa kutekeleza kwa vitendo ushauri wake wa kutaka magari yote ya abiria yaingie stendi ya mabasi.

Akizungumza leo mjini hapa, Mhe. Nyongo amepongeza hatua ya uongozi wa wilaya chini ya Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Aswege Kaminyoge ya kuhakikisha magari ya abiria yanayofanya shughuli zake wilayani humo yanaingia stendi na kulipa ushuru kwa halmashauri.

“Kwa kweli niupongeze sana uongozi wa wilaya kufanyia kazi ushauri huu wa magari yote ya abiria kuingia stendi, hivyo niombe ushirikiano kwa wahusika wote na utaratibu huu uwe endelevu.”

Amesema hatua hiyo itasaidia Halmashauri kupata chanzo cha mapato lakini kubwa ni kuhamasisha na kukuza biashara ya wananchi wa Maswa.

Hivi karibuni wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi, Mhe. Nyongo alishauri kuangalia namna ya kuyafanya magari yote ya abiria yanayofanya shughuli zake ndani au kupita katika wilaya hiyo kuingia stendi ya mabasi hatua ambayo itasaidia kuiingizia mapato Halmashauri hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *