DC SHAKA APIGA MARUFUKU UCHIMBAJI MADINI KWENYE CHANZO CHA MAJI MALOLO

0

Mkuu wa wilaya ya Kilosa mkoani Morogiro Shaka Hamdu Shaka amepiga marufuku shughuli za uchimbaji holela wa madini,kilimo na ukataji miti ovyo kwenye chanzo cha maji Kata ya Malolo wilayani humo.

Dc shaka ameyasema hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji Malolo unaotekelezwa na Ruwasa , ambapo wananchi hao wamesema uchimbaji wa madini katika eneo hilo umekua kero na kusababisha uchafuzi wa maji .

Boazi Igombe ni mkazi wa Malolo anasema wanashukuru Serikali Kwa ujenzi wa mradi huo kwani awali walikua wakipata huduma hiyo umbali mrefu Lakini Bado Changamoto ya shughuli za uchimbaji madini katika chanzo cha maji zinarudisha nyumba jitihada za serikali huku wakihofia Kupata magonjwa ya mlipuko

Baada ya kupata malalamiko hayo Dc Shaka amewataka wananchi kuacha tabia hiyo na atakaye kamatwa hatua za Kisheria zitachukuliwa dhidi yake

Aidha DC shaka amewataka wananchi hao kuwa walinzi wa miundombinu hiyo Ili iwanufaisha Kwa kipindi kirefu kizazi Cha Sasa na kijacho kwani serikali inatumia gharama kubwa kuwafikishia huduma hiyo wananchi

Anasema serikali imekua ikitekeleza ujenzi wa miradi Mbalimbali kwenye sekta ya maji hivyo baadhi ya watu wamekua na wakiharibu miundombinu hiyo.

“dokta samia Suluhu Hasaan amekua akitoa fedha kwenye miradi ya maji hasa wilaya hii ya Kilosa hivyo lazima tutunze miundombinu hii na Kila mtu awe mlinzi wa mwezake”

Kwa Upande wake meneja Wakala wa maji safi na Usafi wa Mazingira (RUWASA) wilaya ya Kilosa Mhandisi Silvia Ndimb amesema ujenzi wa mradi huo umegharimu kiasi cha Shilingi Bil.1 na utawanufaisha Wakazi zaidi elfu 13 wa vijiji vya Malolo A,Malolo B na Chabi.

Mradi wa maji Malolo umejengwa kwa kwa Fedha za COVID 19 na ulianza kutekelezwa mwaka wa fedha 2022/2023 chini ya mkandarasi Jeccs Contruction and Supplies limited na Sasa mradi imekamilika kwa asilia 100 tayari umeanza kutoa huduma kwa Wananchi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *