DC SHAKA AMTAKA MKANDARASI UJENZI UWANJA WA NDEGE MINAPA KUONGEZA KASI

0

Mkuu wa wilaya ya Kilosa shaka Hamdu Shaka amemtaka mkandarasi Kutoka kampuni ya Badr East Afrika inayojenga mradi wa ujenzi wa uwanja ndege Hifadhi ya Taifa Mikumi kuongeza Kasi kwa kufanya kazi usiku na mchana Ili ukamilike kwa wakati.

Dc Shaka ameyasema hayo baada ya kufanya ziara ya kutembelea ujenzi wa mradi huo ambao unajengwa ndani ya Hifadhi hiyo wenye Lengo wa kuongeza idadi ya watalii.

Dc shaka amesema Serikali ya awamu ya sita imekua inatoa fedha kwenye miradi mbalimbali hivyo katika kuendelea kusapoti sekta ya utalii Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha kiasi Cha shilingi bilioni 20.6 kwa ajili ya ujenzi uwanja huo wa ndege.

Aidha ametoa Wito kwa watu mbalimbali kuendelea kutembelea Hifadhi hiyo Ili kuongeza pato la Taifa badala ya kuacha wageni pekee kufanya shughuli za utalii.

Kaimu mkuu wa Hifadhi hiyo ya Mikumi Buka Alfred amesema mradi huo umefikia asilimi 60 Kwa sasa na unatakiwa kukamilika Mwezi Julai mwaka huu.

Amesema kukamilika kwa mradi huo utaongeza idadi ya watalii wanaotumia usafiri wa anga huku akisisitiza kuwa Hifadhi hiyo inafika Kwa njia ya Reli ya kati ,Reli ya Mwendokasi,barabara ya TAZAM.

Naye Herman Mtei Mkuu wa Kitengo Cha utalii Hifadhi ya Mikumi amesema kwa mwaka wa fedha 2023/2024 watalii zaidi ya laki moja na telathini wametembelea Hifadhi hiyo ikiwa ongezeko la asilimi 7 la mwaka 2022/2023.

Kwa upande wake msimamizi wa mradi huo Kutoka upande wa kampuni Bw. Peter Mroso amesema sababu kubwa ya kuchelewa kwa mradi huo ni kutokana na kuwepo Kwa mvua nyingi ambazo zimeyesha Kwa kipindi kirefu hivyo ameahidi kufanya Kazi kwa bidii Ili ukamilike kwa wakati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *