DC LUDEWA ATOA VYETI VYA PONGEZI KWA WAKIMBIZA MWENGE KIWILAYA.

0

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva ametoa vyeti vya pongezi kwa wakimbiza mwenge 6 kiwilaya kama ishara ya kutambua mchango wao wa kizalendo katika mbio hizo za mwenge Wilayani humo.

Akikabidi vyeti hivyo katika kikao cha tathmini ya shughuli nzima ya mwenge wa uhuru uliokimbizwa Wilayani humo Juni 16, mwaka huu na kisha kukabidhiwa Halmashauri ya mji wa Njombe Juni 17, mwaka huu Bi. Mwanziva amesema vijana hao walijitoa sana kwenye kuukimbiza mwenge pasipo kujali changamoto ya vumbi na kukesha wakiwa wamesimama.

“Nawapongeza sana wakimbiza mwenge wetu kiwilaya Basil Eligius Mgaya, Gift Octavian Mwinuka, Paschal Peter Kasoma, Khadija Juma Sefu, Zaliwa Mawazo Sinkala pamoja Bernard Joseph Makotelo kwa uzalendo huu uliotukuka”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *