MHE. NYONGO ACHANGIA KANISA MIFUKO 50 YA SARUJI

0

Mbunge wa Jimbo la Maswa Mhe. Stanislaus Haroon Nyongo amechangia ujenzi wa jengo jipya la Kanisa Katoliki Parokia ya Nyalikungu mjini Maswa kwa kutoa mifuko ya saruji.

Nyongo ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji amekabidhi saruji hiyo kupitia kwa Katibu wake wa jimbo Marco Bukwimba.

Akizungumza na uongozi wa Kanisa hilo, Bw. Bukwimba amesema mifuko hiyo ya awali, ni sehemu ya mchango wa mifuko 100 aliyoahidi kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo.

“Mhe Nyongo kama alivyokuwa ameahidi ataendelea kuchangia ujenzi wa kanisa bila kuchoka, kama vile kanisa linavyoliombea amani Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali yake, bila kuchoka.”

Akizungumza kwa niaba ya kanisa hilo Padre wa Parokia hiyo Bw. Deogratias Ntindigo amemshukuru Mbunge huyo kwa kutimiza ahadi yake ambayo itasaidia katika ujenzi wa Kanisa hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *