UPATIKANAJI WA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA WAFIKIA ASILIMIA 79.6

0

“Napenda kulitaarifu Bunge lako Tukufu na wananchi kwa ujumla kuwa hadi Desemba 2023, hali ya upatikanaji wa huduma
ya maji safi na salama ulifikia asilimia 79.6 katika maeneo ya vijijini na asilimia 90.0 mijini. Kwa ujumla, mafanikio hayo yamechangiwa na kukamilika kwa utekelezaji wa miradi 1,633 ya maji vijijini na miradi 213 ya maji mijini,”

Akiwasilisha Mapendekezo ya serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/25 Leo Alhamisi Juni 13,2024 Bungeni Jijini Dodoma Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema “Serikali iliendelea na utekelezaji wa: Mradi
wa Ujenzi wa mtambo wa kutibu maji Butimba ambao utekelezaji umefikia asilimia 99; Mradi wa Maji Mugango – Kiabakari – Butiama asilimia 99; Mradi wa Maji Same – Mwanga – Korogwe asilimia 92; Mradi wa Maji kutoka Mto
Kiwira kwenda jijini Mbeya asilimia 20; Mradi wa Maji wa Miji 28 asilimia 25; na Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Kidunda asilimia 20,”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *