PATO LA TAIFA LIMEONGEZEKA

0

“Mwaka 2023, Pato halisi la Taifa lilifikia shilingi trilioni 148.3 kutoka shilingi trilioni 141.2 mwaka 2022, sawa na ukuaji wa asilimia 5.1 ikilinganishwa na asimilia 4.7 mwaka 2022, Ukuaji huo ulichangiwa na jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ikiwemo, mikakati ya kukabiliana na athari za vita kati ya Ukraine na Urusi pamoja na uwekezaji wa kimkakati katika miundombinu ya nishati, maji, afya, elimu na usafirishaji; kuongezeka kwa uzalishaji wa madini, hususan dhahabu na makaa ya mawe; na kuongezeka kwa mikopo kwa sekta binafsi iliyochachua shughuli za kiuchumi,”

Akiwasilisha taarifa ya hali ya uchumi kwa mwaka 2023 na Mpango wa maendeleo ya taifa kwa mwaka 2024/25 leo Alhamisi Juni 13,2024 bungeni Jijini Dodoma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Mipango na uwekezaji Prof. Kilila Mkumbo (Mb.) amesema

“Mfumuko wa bei nchini ulifikia asilimia 3.1 katika kipindi kilichoishia mwezi Aprili 2024 ikilinganishwa na asilimia 4.3 katika kipindi kama hicho Mwaka 2023. Aidha, mfumuko wa bei ulifikia wastani wa asilimia 3.8 Mwaka 2023 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 4.3 Mwaka 2022. Kiwango hiki ni cha chini ikilinganishwa na nchi wanachama wa EAC na kipo ndani ya malengo ya kati ya asilimia 3.0 hadi 7.0 na vigezo vya mtangamano,”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *