WANANCHI WAMLALAMIKIA RC SHIGELA WAJAWAZITO KUTOZWA FEDHA HOSPITALINI

0

Wananchi wa Kata ya Bufanka Wilaya ya Bukombe wamelalamika mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Geita kuhusu kuwepo tabaia ya kutozwa fedha pindi wanapoenda kujifungua katika kituo cha Afya cha Bufanka jambo ambalo limekuwa likiwaumiza na kutaka kujua kama serikali inafahamu utaratibu huo wa kutoa pesa mjamzito anapoenda kujifungua.

Wameyasema hayo katika mkutano wa hadhara ulifanyika katika kituo hicho cha Afya Bufanka kilichopo katika kijiji cha Bugelenga ambapo Mkuu wa mkoa huo Martine Shigela alipofika katika kituo hicho kukagua hatua za ujenzi wa hospitali hiyo ndipo wakasema kumekuwepo na faini nyingi hasa mwanamke anapojifungulia njiani na wengine kudai pesa hata kabla hajapatiwa huduma ya kujifungua.

Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Bufanka Winifrida David pamoja na Mganga mkuu wa Wilaya ya Bukombe Deograsia Mkapa wamesema kituo hicho hakijawahi kumtoza mgonjwa pesa bali wanawake wengi wa kata hiyo wamekuwa na tabia ya kujifungulia nyumbani na kusema huduma ya mama kujifungua ni bure nahairuhusiwi mtu kuombwa fedha kwa huduma hiyo.

Hata hivyo Mkuu Huyo wa Mkoa amepiga marufuku mjamzito kuombwa pesa yoyote kwani huduma ya kujifungua na matibabu ya mototo aliye chini ya miaka mitano ni bure na kuwata wananchi endapo wataombwa pesa kwa huduma hizo wapige simu kwa kamanda wa jeshi la polisi Geita ili waliohusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *