WANAWAKE WAASWA KUMJUA MUNGU ILI KUWALINDA WATOTO WAO KIIMANI

0

Waumini wa kanisa la Tanzania Missionary Revival Church (TMRC) mjini Geita wamewataka wanawake wote kujikita katika kujua Mungu zaidi ili kuweza kuwafundisha watoto wao maadili mema na kuepukana na mambo mabaya yanayoikumba dunia ya watoto kujihusisha na vitendo vya kihalifu ikiwemo uvutaji wa bangi, ukahaba pamoja na ulawiti kwa watoto.

Wameyasema hayo katika kongamano la kitaifa la wanawake wa kasina hilo la TMRC lililofanya mjini Geita ambapo kongamano hilo limewakusanya zaidi ya wananwake 300 kutoka kila pande ya Tanzania na kusema kwa sasa mambo machafu mengi yameikumba dunia na lengo la kukongamano hilo ni kuwakumbusha wananwake wajibu wao katika familia zao kwakuwa mwanamke ni mulizi wa familia na jamii kwa ujumla.

Kwaupande wake Mchungaji wa kanisa hilo la Tanzania Missionary Revival Church (TMRC) Askofu Stephano Saguda lililopo mjini Geita amewataka waumini wa kanisa hilo kuliombea taifa hasa katika kipindi ambacho nchini ya Tanzania inaelekea katika uchanguzi wa serikali za mitaa na kuwataka wananchi kujitokeza kuchukua fomu na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwani kila mwananchi anahaki ya kugombea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *