OCD LUDEWA AKABIDHIWA GARI

0

Mkuu wa polisi Wilaya ya Ludewa SSP Deogratius Massawe amekabidhiwa rasmi gari mpya ya Polisi ambayo ni miongoni mwa magari 21 yaliyotolewa na serikali kupitia Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango mnamo tarehe 11/05/2024 wakati wa hafla ya kufungua Kituo cha Polisi Daraja “A” Wilaya ya Kipolisi Mtumba Mkoani Dodoma.

Gari hilo lenye namba za usajili PT 5047 Toyota Land cruiser limekabidhiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Mahamoud Hassan Banga katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa kijiji Cha Ilininda Kata ya Madilu Wilayani Ludewa mkoani humo na kusema kuwa mbunge wa Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga aliwasilisha ombi la kupatiwa gari hilo ili kuweza kurahisisha shughuli za kipolisi katika Wilaya ya Ludewa ambapo serikali ikalipokea ombi hilo na kulifanyia kazi na hatimaye kupatiwa gari hilo.

“Ndugu wananchi mbunge wenu amewezesha kupatikana gari hili hivyo tunamshukuru yeye pamoja na serikali kwa msaada huu kwani litasaidia ufanyajinkazi wa jeshi la Polisi kwakuwa mazingira ya maeneo ya Ludewa yamekaa mbalimbali hivyo gari hili litarahisisha Polisi wetu kufanya doria kwa urahisi na hata itakapotokea tukio la kihalifu itasaidia kufika mahali husika kwa wakati”. Amesema Kamanda Banga.

Aidha kwa upande wake Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ludewa SSP Massawe akipokea gari hilo ameishukuru serikali na mbunge Kamonga huku wananchi wakiipongeza serikali kwa juhudi zilizofanyika kwani ulinzi na usalama utaenda kuimarika katika Wilaya yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *