KUELEKEA UZINDUZI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME IFAKARA, HIVI NDIVYO WADAU WANAVYOUZUNGUMZIA MRADI HUO

0

Wakazi wa Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro wameishukuru na kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kukamilika na kuanza kutumika kwa kituo cha Kupoza umeme cha Ifakara.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi hao wamesema kuwa, zamani walikuwa na changamoto kubwa ya kukatika katika kwa umeme katika eneo hilo hali iliyoathiri shughuli zao za kiuchumi na upatikanaji wa huduma muhimu.

Kituo hicho cha Kupoza Umeme cha Ifakara kimejengwa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa Ufadhili wa Umoja wa Ulaya ambapo mpaka kukamilika kwake, jumla ya fedha za Kitanzania Bilioni 25 zimetumika.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko na Balozi wa Umoja wa Ulaya, Mhe. Christine Brau wanarajiwa kuzindua rasmi Kituo hicho, Ijumaa, tarehe 31 Mei, 2024.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *