WADAIWA SUGU NHC KUTAJWA KWENYE VYOMBO VYA HABARI

0

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesema Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) bado linakabiliwa na changamoto ya Wadaiwa sugu wa kodi ya pango, miradi ya ukandarasi na Wanunuzi wa nyumba kutokukamilisha malipo yao kwa wakati, hivyo Shirika limeweka mikakati mbalimbali ili kukabiliana na changamoto ikiwemo kuvunja mikataba ya upangaji kwa Wapangaji
waliokaidi kulipa madeni yao na kuwaondoa kwenye nyumba na kukamata mali zao kwa ajili ya kuuza ili kufidia madeni yao pia kuwatangaza Wadaiwa sugu katika vyombo vya habari.

Akiwasilisha Bungeni Jijini Dodoma Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka 2024/2025 leo May 24,2024, Silaa amesema “Mkakati mwingine ni kuingia mikataba na Wapangaji ili kuwaruhusu kulipa madeni yao kwa awamu, pia kuhakikisha kuwa kila Mpangaji mpya anayepangishwa analipa amana ya pango ya miezi mitatu (security deposit)”

“Mkakati mwingine ni kuingia makubaliano na Credit Information Reference Bureau ili kusajili majina ya Wadaiwa sugu na kuwanyima fursa ya kupata mikopo katika taasisi za fedha”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *