TLS, ASASI ZA KIRAIA KUPELEKA ELIMU KWA JAMII KUHUSU HAKI NA UHURU WA KUJIELEZA

0

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Imeelezwa kuwa Tanzania kama nchi inayotajwa kujiendesha kidemokrasia, imekuwa ikipitia vipindi tofauti tofauti hali inayopelekea wakati mwingine haki na Uhuru wa kujieleza kuminywa au kukandimizwa katika jamii.

Kutokana na hali hiyo Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) kimeona haja ya kuwajengea uwezo Asasi za Kiraia kuhusu namna ya kutafuta kusaidia serikali na wananchi kwenye masuala yote yanayohusu sheria ili nao wawe na uelewa sahihi juu ya haki zao .

Akiongea na waandishi wa habari leo Mei 20,2024 jijini Dodoma Afisa miradi chama cha Wanasheria Tanzania TLS Victor Mbulingwe amesema moja ya malengo ya kuanzishwa kwa chama hicho ni kusaidia serikali na bunge katika Mambo yote yanayohusu sheria na utendaji kazi wake.

Mbuligwe amesema, “TLS kazi yetu kubwa ni kuhakikisha utekelezaji wa sheria au kwa lugha nyengine utekelezaji kazi sheria unakuwa upo sawa sawa na haki za watu waliopo katika nchi inapatikana,lengo letu ni kuhakikisha jamii inajivunia haki “amesema .

Licha ya hayo ameongeza TLS imeona vyema kuwasaidia kwa kuwajengea uwezo Asasi hizo za kiria katika masuala ya Uhuru wa kujieleza ambapo Uhuru wa kujieleza unalindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kifungu cha kwanza kidogo cha 18 “abcd”.

Amesema kila mtu anao uhuru wa kutoa maoni yake, kupokea taarifa kutafuta taarifa, kusambaza taarifa bila kujali mipaka ya nchi lakini pia kupewa taarifa yoyote katika nchi huku akifafanua kuwa taarifa hizo zitolewe kwa kufuata misingi ya utamaduni wa mwafrika.

” Ili kuhakikisha tunaipa jamii tunayoishi kile wanachostahiki kukipata tumeona tuwajengee uwezo hawa Asasi za kiria ili nao waende kutoa elimu katika jamii zao huko chini, tunaimani kupitia jukwaa hili jamii itafikishiwa matumizi ya sheria na kila mwanajamii atafaham namna ya kudai na kutenda haki, “amesisitiza

Pamoja na mambo mengine Afisa miradi huyo wa TLS amefafanua kuwa mbali na kutoa mafunzo hayo kwa Asasi za kijamii, wana mpango wa kuandaa mafunzo kama hayo kwa makundi mengi ya kijamii .

Kwa upande wake Rose Ugulumu Kaine Mkurugenzi wa shirika la Biashara na haki za Binadamu Tanzania amesema Mafunzo yanayofanywa na TLS yatawasaidia namna bora ya kufanya kazi katika kipengele cha haki ya kujieleza katika jamii.

“Sio Sisi tu watu tunaowafundisha jamii lakini na watu kujua haki zao za kujieleza kulingana na sheria ,hapa leo tunafundishwa jinsi gani ya kujieleza na Mambo mbalimbali tunayofanyia kazi na haki ya kujieleza na sheria hiyo kwa ujumla, “amesema Kaimu Mkurugenzi huyo

Amesema kuwa dhana ya kujieleza lazima iwe na mipaka kwani huwezi kujieleza kinyume na sheria kusiguse utu wa mtu hivyo kila mtu anapaswa kujua kuwa anapojieleza lazima asimame kwenye misingi bora kama watetezi wa haki za binadamu .

“Tumepewa Uhuru wa kujieleza lakini tuzingatie masuala sheria, masuala ya mahusiano ya kijamii masuala ya Mila na desturi zetu ili tuweze kuleta ule Uhuru wetu uweze kutumika kifasaha na kuleta maendeleo katika jamii yetu, ” Amesema Kaimu Mkurugenzi huyo Rose

Naye Omary Lubuva kutoka Shirikisho la watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) ametumia nafasi hiyo kuipongeza TLS kwa kuwajengea uwezo hasa katika sheria ya haki ya kujieleza kwani waliowengi wa Tanzania sio Wanasheria kwa kiasi kikubwa na uelewa wao juu ya kujieleza

“Kupitia mafunzo hayo yaliowakusanya makundi tofauti tofauti yatasaidia katika kuwafikia wananchi kutambua na kuifahamu sheria ya haki ya kujiekeza,sheria hiyo ndio inayosaidia kuzifikia au kuzielewa sheria nyingine na hatimaye kusaidia haki kupatika, ” amesisitiza.

Amefafanua kuwa ,”Tunaimani baada ya hapa na Sisi kama viongozi SHIVYAWATA tutakwenda kuwajengea uwezo ili mwisho wa siku kuweza kudai haki zao na kutumia vizuri maarifa ya sheria ya Uhuru wa kujiekeza,” Amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *