MZABUNI HATIANI KWA RUSHWA, BUKOBA

0

Mahakama ya Wilaya Bukoba imemtia hatiani mzabuni Consolatha John Balole ambaye ni Meneja wa Kampuni ya ZainAbbas Enterprises.

Mshtakiwa ametiwa hatiani na kuamriwa alipe faini ya shilingi Laki Tano au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela, kwa kosa la Hongo k/f 15 (1) (a) na (b) PCCA.

Hukumu hiyo dhidi ya Consolatha John Balole katika shauri la rushwa  Namba 13177/2024 imetolewa na Mhe Hakimu Flora Kaijage wa Mahakama ya Wilaya ya Bukoba Mei 17, 2024.

Kwamba kati ya Mwezi Machi na Septemba 2022  mshitakiwa alijipatia manufaa isivyo stahili hongo ya sh 15,536,000/= katika manunuzi ya vifaa vya ujenzi wa nyumba ya makazi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, fedha ambayo amekwisha rejesha katika ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Kagera.

Mshtakiwa amelipa faini na kuachiwa huru.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *