AZANIA BANK KUWAWEZESHA WAKULIMA WA CHAI KUPITIA AKAUNTI YA MAALUM

0

Benki ya Azania hii leo imetiliana saini na Chama kilele cha Ushirika wa Wakulima wa Chai, TASTGCU, mkataba ambao Benki ya Azania itafungua akaunti maalum itakayoitwa Dunduliza ambayo itahifadhi fedha za jumla za makato ya mauzo ya Chai kutoka kwa wakulima kupitia vyama vya Ushirika (AMCOS).

Fedha hizo zitaviwezesha vyama vya Ushirika kutatua changamoto mbalimbali zinazolikabili zao la Chai nchini ikiwemo ununuzi wa Mbolea na Pembejeo, Miche bora ya Chai na ufunguzi wa viwanda vidogo vya kuchakata zao la Chai hivyo kuliwezesha zao hilo kuongezeka thamani kwenye soko la dunia. Haya yote yatafanyika chini ya usimamizi wa Bodi ya Chai nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *