SERIKALI YAANZA KUCHUKUA HATUA KALI KUKOMESHA WIZI MITANDAONI.

0

Serikali imesema tayari imechukua hatua kadhaa kwa ajili ya kuweka mazingira salama kwa wananchi hususani kwenye mitandao ambapo Serikali imetunga Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya mwaka 2022 ambayo lengo kuu ni kuweka utaratibu wa kuhakikisha wakusanya taarifa wote wanafuata misingi ya kulinda taarifa za mwananchi. Aidha, Serikali ilianzisha Kitengo cha Uhalifu wa Mitandao chini ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa makosa ya mitandao ikiwemo wizi wa aina yoyote kwenye mtandao na kuandaa majalada ya kufungulia mashtaka kwa kusaidiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

Kauli hiyo imetolewa leo 15, April 2024 Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Habari, Mawasiliano, na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye wakati akijibu Swali la Mbunge wa Buhigwe Mhe. Kavejuru Felix aliyetaka kujua Je! Serikali imachukua Hatua gani kukomesha wizi Mitandaoni.

Waziri Nape amejibu kuwa Serikali ilitunga Sheria ya Makosa ya Mitandao na Sheria ya Miamala ya Kielektroniki kwa lengo la kutambua miamala inayofanyika kimtandao lakini pia kutambua kisheria makosa yanayofanyika kwenye mitandao ili kuweza kuchukua hatua stahiki yanapobainika makosa hayo. Pia katika kujenga mazingira salama ya kisheria,

Katika hatua nyingine, Serikali kwa kushirikiana na Watoa Huduma wa Simu za mkononi imeanzisha mfumo kupitia namba “15040” wa kupokea na kuzifungia namba ambazo zimeripotiwa na kuthibitika kutuma ujumbe au kupiga simu za utapeli. Baada ya kuthibitisha namba hizo kufanya vitendo hivyo, namba husika hufungiwa, kitambulisho cha NIDA kilichotumiwa kusajili namba husika kufungiwa kusajili na kifaa kilichotumika (simu) pia kufungiwa ili kisifanye kazi.

“Serikali itaendelea kuongeza jitihada za kuelimisha umma namna nzuri ya kutumia TEHAMA ili kuendelea kudhibiti matukio ya utapeli na wizi wa kimtandao kupitia simu za mkononi.” Ameeleza Waziri Nape

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *