BILIONI 710 KUKARABATI BARABARA ZA WILAYA

0

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Mhe. Zainabu Katimba (Mb) amsema Serikali inatambua umhimu mkubwa sana wa Barabara za Wilaya na kupelekea kuongeza Bajeti za Barabara za Wilaya (TARURA) kutoka Bil. 275 mpaka Bil. 710 ili kuhakikisha Wananchi wanazifikia huduma mbalimbali kwa urahisi.

Mhe. Katimba amesema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Lushoto Mhe. Shabani Omari Shekilindi alitakakujua Je Serikali inampango gani wa dharura wa kutengeneza Barabara za Maligwi, Wekangwa, Makole na Mbeleyi zilizoathiriwa na mvua ili kurejesha huduma kwa Wananchi?

“Serikali inatambua umhimu mkubwa sana wa Barabara za Wilaya na kupelekea kuongeza Bajeti za Barabara za Wilaya (TARURA) kutoka Bil. 275 mpaka Bil. 710 yote hii ni kuakikisha kwamba miundombinu ya Barabara za Wilaya inakuwa vizuri na kuwasaidia Wananchi kufikia huduma ili waweze kujijenga kiuchumi kupitia shughuli zao za uzalishaji”

Aidha Mhe. Katimba amesema kutokana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi ya mara kwa mara na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya Barabara Serikali imeanza kutumia Teknolojia Mbadala katika ujenzi wa Barabara za Wilaya kwa kutumia Mawe ambayo ni gharama nafuu na hudumu kwa muda mrefu zaidi na majaribio yameanza kwenye baadhi ya maeneo ili kuona ufanisi na ubora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *