MWENYEKITI KAWAIDA AKUTANA NA WANAMZIKI WA VIJANA JAZZ

0

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Komredi Mohammed Ali Kawaida (MCC) amekutana na kufanya mazungumzo na Wasanii wa Bendi ya Vijana Jazz tarehe 14 Mei, 2024 Vijana Social Hall Kinondoni.

Komredi Kawaida amewapongeza kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya ya kutoa burudani Maeneo mbalimbali pale wanapopata nafasi na kuwaahidi kuwaunga Mkono kwenye kila hatua ya maboresho wanayotazamia katika kuiinua Vijana Jazz Zaidi.

“Niwapongeze sana kwa kazi nzuri mnayoifanya na hatua mnazochukua Kila mnapopata nafasi ya kualikwa kutoa burudani kwenye Mikutano mbalimbali, Mnafanya Vizuri sana na Sisi Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tutaendelea kuwaunga Mkono kwenye kila hatua mnazochukua za kuboresha Bendi hii iwe ya kisasa Zaidi.

Aidha Ndugu Kawaida alifanikiwa kusikiliza baadhi Nyimbo Mpya za Bendi hio ambazo zilimvutia na kuwaahidi kuwasaidia kuingia kambini kutengeneza Nyimbo Bora zaidi na za kisasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *