TIC KINARA TUZO ZA TAASISI BORA YA UWEKEZAJI AFRIKA

0

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kupokea tuzo hiyo Dkt. Kida, alisema tuzo hiyo imekuja wakati mwafaka na ni tunu kwa taifa kwani inaakisi jitihada za Serikali za kuimarisha mazingira ya biashara nchini zinazoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“tuzo hii inaongeza imani kwa wawekezaji na sisi Serikali hasa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji tutaendelea kuvutia uwekezaji ili kuzalisha ajira na kukuza uchumi wa nchi yetu” Alisema Dkt. Kida.

Katika kinyang’anyilo cha tuzo hiyo, inayotolewa na waandaaji wa Mkutano wa Mwaka wa Uwekezaji (AIM Congress) unaoendelea Abu Dhabi, TIC imezipuku taasisi mbalimbali za Uwekezaji za matiafa ya Afrika kwa kuwa na ongezeko chanya katika vigezo vya Usajili wa Miradi, Thamani ya Uwekezajia na Idadi ya ajira zinazotokana na shughuli za Kituo hicho.

Kwenye kigezo cha usajili wa miradi, kwa kipindi cha Januari 1, 2023 hadi Desemba 31, 2023, TIC iliongeza miradi inayosajiliwa hadi 526 kutoka 293 iliyosajiliwa katika kipindi kama hicho mwaka 2022, ikiwa ni ongezeko la 79.5%.

Aidha, katika kigezo cha thamani ya uwekezaji, kati ya Januari 1, 2023 na Desemba 31, 2023, thamani ya uwekezaji uliyowezeshwa na TIC iliongezeka kufikia Dola za Marekani milioni 5,720.36 kutoka Dola za Marekani milioni 4,547.70 zilizorekodiwa kipindi kama hicho 2022, ikiwa ni ongezeko la asilimia 25.8.

Vile vile, idadi ya ajira zilizoundwa kutokana na shughuli za TIC kati ya Januari 1, 2023 hadi Desemba 31, 2023, zimeongezeka hadi 137,010 kutoka 40,889 zilizorekodiwa kipindi kama hicho mwaka 2022 ikiwa ni ongezeko la 235.1%.

Taasisi mbalimbali ulimwenguni huwania tuzo ya ‘taasisi bora ya uwekezaji’ inayotolewa sanjali na tuzo nyingine za uwekezaji tangu 2013 kama utambuzi unaothaminiwa na wingi wa miradi bora ya Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Kigeni (FDI) kutoka kila eneo la dunia ambalo Wakala wa Kukuza Uwekezaji (IPA) ilivutia katika mwaka husika.

Dkt. Kida, yupo Abu Adhabi kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji anaungana na watu mashuhuri, wakiwemo Mawaziri, Maafisa wa Serikali, na watoa maamuzi kutoka kote ulimwenguni, pamoja na wawekezaji wakuu, h zaidi ya 12,000 kutoka zaidi ya nchi 175.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *