ASILIMIA 95 YA WAKAZI MIJINI WANAPATA MAJI SAFI NA SALAMA

0

“Upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo ya mijini umefikia wastani wa asilimia 90 mwezi Desemba 2023 kutoka wastani wa asilimia 88 mwezi Desemba, 2022. Ongezeko hilo limetokana na kukamilika kwa miradi ya maji 85 inayohudumia wakazi 4,641,505 wa maeneo ya mijini.

“Dhamira ya Serikali ni kuona, zaidi ya asilimia 95 ya wakazi wa mijini wanapata huduma ya maji safi na salama ifikapo mwaka 2025. Kwa upande wa huduma ya uondoshaji majitaka, mtandao unaotoa huduma hiyo nchini umefikia kilomita 1,455.93 mwezi Aprili, 2024 na idadi ya wateja waliounganishwa katika mtandao imefikia 58,650.

“Kwa maeneo yasiyofikiwa na mtandao, huduma ya majitaka hutolewa na magari maalum ambayo huyakusanya na kutibiwa kwenye mabwawa ya kutibu majitaka” Mhe. Jumaa Aweso, Waziri wa Maji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *