BUNGE LAIDHINISHA TRILIONI 1.97 KULETA MAGEUZI SEKTA YA ELIMU
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania laidhinisha zaidi ya shilingi Trilioni 1.97 zilizoombwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya kutekeleza vipaumbele vitano vya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 ili kuleta mageuzi ya Elimu nchini.
Vipaumbele hivyo ni pamoja na;
(i)Kuendelea na utekelezaji wa sera na mitaala, mapitio ya sheria na kuandaa miongozo ya utoaji elimu na mafunzo nchini
(ii) Kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (amali na amali sanifu).
(iii) Kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya msingi, sekondari na ualimu.
(iv) Kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya juu na kuendeleza tafiti, matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu.
(V) Kuendelea na utekelezaji wa Sera na Mitaala, Mapitio ya Sheria na kuandaa Miongozo ya Utoaji Elimu na Mafunzo Nchini.
Mwelekeo wa Wizara ya Elimu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 ni kuweka mkazo kwenye Elimu ya Ujuzi (Skillis Oriented) ili kuwawezesha wahitimu wa ngazi mbalimbali za Elimu kujiajiri na kuajiri wengine.