VIFAA VYA MAABARA VYA SHULE 1,322 NA VYUO 13 VYA UALIMU KUNUNULIWA

0

Waziri wa Elimu, Sayansi, na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali itanunua vifaa vya maabara kwa ajili ya shule za sekondari 1,322 na vyuo 13 vya ualimu pamoja na vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika vyuo 35 vya ualimu.

Waziri Prof. Mkenda ameyasema hayo mapema leo 07 Mei, 2024 Bungeni wakati akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti Wizara ya Elimu, Sayansi, na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.

“Vilevile, itanunua vifaa vya kujifunzia na kemikali kwa ajili ya kufundishia masomo ya sayansi kwa wanafunzi wa elimu kwa njia mbadala kwa hatua ya I na II.“ amesema Prof.Adolf Mkenda waziri wa Elimu sayansi na teknolojia.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *