SERIKALI YATANGAZA VIPAUMBELE VITANO SEKTA YA ELIMU 2024/2025
“Vipaumbele vya Wizara Elimu kwa mwaka wa fedha 2024/25 ni kama vifuatavyo:
Kuendelea na utekelezaji wa sera na mitaala, mapitio ya sheria na kuandaa miongozo ya utoaji elimu na mafunzo nchini
Kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (amali na amali sanifu);
Kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya msingi, sekondari na ualimu;
Kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya juu; na kuendeleza tafiti, matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu.
Kuendelea na utekelezaji wa Sera na Mitaala, Mapitio ya Sheria na kuandaa Miongozo ya Utoaji Elimu na Mafunzo Nchini“ – Prof Adolf Mkenda waziri wa Elimu Sayansi na teknolojia