SERIKALI KUJENGA SHULE 100 MPYA ZA AMALI

0

Aidha, Prof. Mkenda amesema ujenzi wa shule za amali utapewa kipaumbele katika maeneo ambayo hayana vyuo ya mafunzo ya ufundi stadi

Kwa upande mwingine, Waziri huyo wa Elimu amesema serikali
itaendelea na ujenzi wa vyuo 65 vya mafunzo ya ufundi stadi, kati ya hivyo 64 ni vya wilaya na kimoja ni cha ngazi ya Mkoa wa Songwe.

Vilevile, Serikali imeongeza vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika vyuo 29 vilivyokamilisha ujenzi na
itaendelea na ujenzi wa miundombinu ya nyongeza katika vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi kama vile Ndolage-Muleba, Ileje, Newala, Ngorongoro, Gorowa – Babati, Urambo, Kasulu, Mabalanga – Kilindi, Nkasi na Kanadi – Bariadi, ili kuviwezesha vyuo hivyo kufikia viwango vya msingi vya utoaji wa mafunzo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *