TIC, AZANIA BANK WAZINDUA KITUO CHA KISASA CHA KUTOLEA HUDUMA

0

Katika kuongeza ufanisi na kuendelea kutoa huduma kisasa zaidi zenye kiwango cha hali ya juu, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Benki ya Azania, leo tarehe 4 Mei, 2024 wamezindua kituo cha kisasa cha kutolea huduma kwa wateja chenye muonekano wa daraja la kwanza (Premium Lounge) na teknolojia ikiwemo vitendea kazi vya kisasa.

Kituo hicho ambacho kimejengwa kwa ufadhili wa Benki ya Azania kinapatikana ndani ya ofisi za makao makuu ya kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Jijini Dar es salaam.

Uzinduzi huo umefanywa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *