MREMBO MISS TANZANITE AGAWA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI

0

Mrembo Miongoni mwa Washindi wa Taji la Miss Tanzanite Manyara 2023/2024 Miss Eva Godwin ametoa msaada wa Taulo za Kike kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nagulo iliyopo Wilayani Bahi Mkoani Dodoma wanaoanzia Darasa la 5-7.

Akizungumza mrembo huyo amesema hii sio mara ya kwanza kwake kutoa misaada kupitia Taasisi yake ya Fountain Charity foundation huku wanafunzi wakimshukuru Miss Eva kwa msaada huo wa Taulo.

Katika zoezi hilo Miss Eva aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Natha’s Entertainment na Mwandaaji wa Miss Tanzanite Manyara Bi. Aminatha Shamghe ambapo yeye amewataka warembo kuwa na tabia ya kurudisha kwa jamii na sio kukaa na mataji kwa kuyatumia vibaya na kufanya mambo yasiyo na maadili katika mitandao ya kijamii.

Kushoto ni Bi. Aminatha Shamghe Mkurugenzi wa Natha’s Entertainment na mwandaaji wa Shindano la Ulimbwende la Miss Tanzanite Manyara akiwa na Miss Eva Godwin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *